Monday, June 10, 2013

0

MASHUJAA BAND KALA JEREMIAH NA OMMY DIMPOZ WANG'ARA KTMA



Usiku wa jana ulikuwa ni usiku wa furaha sana kwa Mashujaa Band ambao waliongoza kwa kuondoka na tuzo nyingi kuliko wasanii wengne. Mashujaa ambao wanafanya vizuri na wimbo wao wa ''Kidole Risasi'' waliondoka na kura 5 ikiwa ni pamoja na msanii bora wa kiume band Charz Baba, mtunzi bora a mashari ya band Charz Baba, rapper bora wa band Furguson, wimbo bora wa band Risasi Kidole na tuzo ya tano waliichukuwa kupitia category ya band bora ya mwaka huku wakiwatupa kule Twanga Pepeta, Mapacha Watatu na Msondo Ngoma

Wakati huo, upande wa hiphop, Kala Jeremiah aliondoka na tuzo tatu na kuwaacha chin
i akina Fid Q,Stamina na wengineo, ambapo aliondoka na tuzo ya  msanii bora wa hiphop, mtunzi bora wa mashairi ya hiphop na wimbo bora wa mwaka ''Dear God''


King Crrazy GK akitoa salam zake baaada ya kupigiwa shangwe la hatari alipopanda jukwaani kutoa tuzo ya mssanii bora wa Hiphop

 
Ommy Dimpoz nae, alisepa na tuzo tatu , wimbo bora wa kushirikiana ''me and you'', video bora ya mwaka ''Baadae'' na wimbo bora wa bongo pop


kutoka arusha, Jambo Squad waliwakilisha vizuri baada ya kuchukua tuzo ya kundi bora la muziki wa kizazi kipya

Mrisho Mpoto ameondoka na tuzo ya wimbo bora wenye vionjo vya asili ''chocheeni kuni''

mtayarishaji boa wa mwaka ni Man Walter


Ben pol aliondoka n tuzo ya mtunzi bora wa muziki bongo fle
va
wengine ni pamoja na Diamond ambae aliondoka na  tuzo ya msanii bora wa kiume na msanii bora wa kiumee bongo fleva. msanii anaechipukia ''Ally Nipishe'', mtayarishaji anaechipukia ''Mensen Selector, wimbo bora wa hiphop ''nasema nao'' Ney wa mitego, wimbo bora wa Zouk/Rhumba ''ni wewe'' Amini, wimbo bora wa Africa mashariki ''Valu valu'' Chameleon, msanii bora wa kike ''Jay Dee

0 comments: