Friday, February 15, 2013

0

JINSI YA KUPUNGUZA MWILI KUONDOKANA NA MARADHI MBALIMBALI..

Hii sio ya kitaalamu bali ni mimi ninavyofanya na ndio inayonisaidia kupunguza tumbo.
Kwasababu vitu vya formula mimi huwa siwezi kuvifuata na huwa naviona vigumu sana kwahiyo huwa najaribu kuishi vile ninavyoweza.

Na kizuri zaidi ni kwamba hii sio diet ya kujinyima.
Ila unaweza usifanikiwe pia kutokana na mwili wako kwakua tumeumbwa tofauti lakini unaweza kujaribu kama itafanya kazi


Tukianza na asubuhi nikiamka mimi kama Mzizimkavu, naanza kunywa maji glass 3 ya Uvugu vugu kabla ya kupiga mswaki.
Na nikiisha amka nakunywa maji ya uvugu vugu yaliokamuliwa ndimu au limao glass zingine tatu kabla ya kunywa Chai.
Ukizoea maji ni matamu kuliko hata Bia
Kuwa Teja wa Maji kuna raha yake pia

Mimi napenda vitu vichachu kwahiyo maji saa zingine naya hisi kama yamepooza ila nikikamulia ndimu/limao kwenye maji ya uvuguvugu hata nisipoweka sukari yanaleta ladha fulani hivi
Ukiweza kunywa maji ya uvugu vugu kila wakati unapohisi kiu ya maji itakuwa vizuri au hata mara tatu kwa siku angalau

Si mpenzi sana wa Chai kwakuwa sipendi kabisa vitu vya sukari, lakini siku ninapo amua kunywa chai huwa nakunywa yenye tangazwizi nyingi sana na badala ya kutumia sukari huwa naweka asali...... Ila unaweza kutumia viungo vingine mbali mbali vya ki pwani (masala)


Asali


Kwa kifungua kinywa Sausage za kuchemsha au kama utakaanga iwe kwa mafuta yasiozidi kijiko kimoja kikubwa cha kulia (nashauri ya alizeti au olive)

Mayai ya kuchemsha si mabaya pia kwa kufungua kinywa
Kumbuka mimi huwa sifanyi diet hivi ndivyo ninavyokula na inasaidia

Badala ya kutafuna Sambusa, Popcorn na cookies au chocolate kila wakati bora muda wako uelekeze kwenye matunda, kama huwezi kupitisha lisaa bila kuweka kitu mdomoni


Mchana unaweza kupiga bakuli la mchemsho wa ndizi, ziwe Bukoba au za kule kwetu Moshi zote sawa kwakuwa mchemsho hauna mafuta kabisa unajilia kadri utakavyotosheka

Kuku Choma ni chakula kingine ambacho kinanifaa nyakati za mchana, lakini haswa hupendelea Kuku wa kienyeji ambao hawakukuzwa kwa madawa
Mara nyingi usiku naipotezea tu, pengine nalalia glass 2 za wine au beer kadhaa zisizozidi 3
Au Kuku wa kienyeji wa kuchemsha aliewekwa chumvi na ndimu na ka ndizi kamoja ka kuchemsha au kukaanga kwa mafuta kidogo sana


Ugali naupenda sana na huwa najiachia nao siku za kujiharibu
Lakini kumbuka wanga sio kitu cha kukiendekeza sana hasa unapotaka kutoa kitambi
Nikiona kinachomoza, napunguza maswala ya ugali.
Japo kwangu ni ngumu siku ipite bila Ugali, ila kumbuka miili inatofautiana... naweza nikala ugali mwaka mzima mwingine akala wiki akafumuka
So usinifatishe ila jaribu kupunguza au uepuke kama utaweza

Tumbo liko hapa sasa!!!!!
Hili ndio tatizo lililonikuta mpaka mkaona ile ishu imechomoka siku ya Birthday yangu


Kwakweli chips ni tamu hasa kwa sisi tunaofanya kazi za usiku ukirudi umejichokea unavamia tu



Unakuta unafululiza hata mwezi unazila kisha unaenda kulala
Japo tunapenda chips vumbi ila tuwe na kipimo isizidi, isiwe kila siku
Ukijumlisha na bia, daaah!! dah!!!!!! dah!!!!! shughuli imeisha



No. 1 enemy kwa vitambi vya wanawake ni hii kitu
Kula angalau mara moja kwa wiki tafadhali kama huwezi kuacha kabisa




Wenye kuweza kufanya sit ups pia fanyeni japo najua mazoezi ni magumu sana na yanatia uvivu hasa unapokuwa na kazi nyingi



Maji ni kitu cha lazima na cha kila siku
Ukiweza kunywa maji ya uvuguvugu Asubuhi, Mchana na Usiku utafanikiwa japo kidogo



Narudia hii sio Diet ya kitaalam ni jinsi ninavyo ishi mimi, jaribu kama utaweza kufanikiwa kwa wale walioniomba ushauri.
Ila kama mwili wako ni mkubwa sana pia jaribu kupunguza kipimo cha chakula unachokula kila siku, ila usijinyime sana.

Mboga mboga kibao kila siku ukiamua mchana na jioni. Ni muhimu sana

0 comments: