Tuesday, June 11, 2013

0

MSANII BORA WA HIPHOP ATANGAZA KUGAWA TUZO YAKE KWA MAREHEM ALBERT MANGWEA


Leo hii nimepita ukurasa wamsanii bora wa hiphop, mtunzi bora na aliechukua tuzo ya wimbo bora
wa hiphop, Kala Jeremiah, na kukutana na ujumbe aliouandika akitangaza kutoa tuzo moja kwa marehem Albert Mangweha a.k.a Ngwea na kuikabidhi kwa mama mzazi wa marehem Albert Mangwea.

''tAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA UMMA KWA UJUMLA.

mIMI KAMA MSANII BORA WA HIP HOP KWA MWAKA HUU NAPENDA KUCHUKUA MUDA HUU KUWATANGAZIA WATU WOOTE KUWA. KATIKA TUZO TATU NILIZOCHUKUA MOJA NAIKABIDHI KWA ALBERT MANGWEA.YANI NI TUZO YA MANGWEA NA NITAIPELEKA KWA MAMA MZAZI WA MANGWEA MOROGORO.

NIMEAMUA HAYO KWA KUWA HAYATI ALBERT MANGWEA ALIKUWA ANAFANYA MZIKI AMBAO UKO UPANDE AMBAO MIMI NIMESHINDA TUZO TATU YANI HIP HOP.

TUZO NILIYOAMUA KUMPA MANGWEA NI TUZO YA MSANII BORA WA HIP HOP. KWA KUWA ALIKUWA ANASTAHILI PIA KUITWA HIVYO

TUZO HII NAAMINI ITAKUWA UKUMBUSHO MHIMU SANA KWA FAMILIA YAKE.LAKINI PIA ITAKUWA INAONYESHA MSHIKAMANO WETU KAMA WASANII WA HIP HOP.''

POPOTE ULIPO KAMA WEWE NI SHABIKI WA HIP HOP TAFUTA NJIA YOYOTE YA KUENDELEA KUMUENZI NDUGU YETU

MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI HIP HOP.

0 comments: