Saturday, October 6, 2012

0

Darasa la saba Mbeya wakabiliwa na uhaba wa kalamu maalum za kujibia mitihani

Posted in ,

Zaidi ya wanafunzi 71,400 wa Shule za msingi 1081 zilizopo mkoani Mbeya wameanza rasmi mtihani wa Taifa wa kuhitimu elimu ya msingi chini ya wasimamizi wa mitihani hiyo 3,160 waliosambazwa katika wilaya nane za mkoa huo.

Afisa elimu wa mkoa wa Mbeya Juma Kaponda amesema pamoja na kuanza kwa mtihani mkoani humo, kumetokea uhaba wa kalamu maalum za kujibia mitihani hiyo kwa kutumia teknolojia ya OMR na kwamba jitihada za kuzitafuta zitazaa matunda.

Ikiwa ni mara ya kwanza kwa wanafunzi wa shule za msingi kutumia teknolojia mpya ya kujibu mitihani kwa kuweka vivuli kwenye eneo la majibu, ambapo baadhi ya wazazi na walezi wameingia hofu na mfumo huu mpya.

Hosea Cheyo, TBC Mbeya.

Afisa elimu wa mkoa wa Mbeya,Juma Kaponda


0 comments: