VURUGU ZA WAISLAMU MBAGALA,MAPEMA LEO HUKO WAMEVAMIA KITUO KIDOGO CHA POLISI , MABOMU YA MACHOZI YALINDIMA!
Vurugu zilizotokea Mbagala Kizuiani ambapo baadhi ya Waislamu wameandamana kupinga kitendo cha kijana mmoja kukojolea Quran. Kwa sasa mabomu ya machozi yanapigwa ili kuwatawanya waandamanaji hao ambao wamezingira kituo cha Polisi wakitaka kijana huyo atolewa la sivyo watakichoma moto kituo hicho.
Chanzo cha fujo hizo; ni manishano ya madogo wawili wenye imani tofauti mmoja akimwambia mwenzake kwamba eti ukikojolea msaafu unakua chizi yule dogo mwingine kaukojolea kweli na hajawa chizi, Yule mwenzake alivyoona kashindwa ikabidi aende msikitini akawatonya waislamu kwamba kuna dogo kakojolea msaafu, Si unajua tena wakatoka waislamu wenye siasa kali wakataka kumuua dogo polisi wameingilia kati na kumuokoa huyo dogo sasa ni vita ya mabomu ya machozi ya Polisi na mawe yanayorushwa na waislamu, Hali sio shwari kabisa magari kibao yamevunjwa vioo
0 comments: