WAFUASI WA SHEIKH PONDA WAKAMATWA WAKIANDAMANA JIJINI DAR ES SALAAM
Polisi wakiwa wamemshikilia mmoja wa wafuasi wa Sheikh Ponda baada ya kukamatwa akiandamana jana katika eneo la kituo kikuu cha polisi Kati jijini Dar.
Mmoja wa wafuasi wa kikundi cha waislamu wenye imani kali akidhibitiwa na polisi mara baada ya kukamatwa jana katika kituo kikuu cha polisi Kati wakijaribu kuandamana ili kushinikiza kiongozi wao Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Sheikh Ponda Issa Ponda kuachiwa na jeshi la polisi mara baada ya kukamatwa jijini Dar es salaam kwa kudaiwa kusababisha vurugu.
Polisi wakiwa tayari kwa kudhibiti maandamano hayo katika kituo kikuu cha Reli karibu na polisi kati jijini Dar es salaam jana mchana.
0 comments: