Kuna aina ngapi za dawa za kulevya?
Tunatofautisha
dawa za kulevya katika makundi mawili. Zile zinazokubalika na zile
zisizokubalika kisheria. Tanzania, dawa za kulevya zinazokubalika
kisheria ni pamoja na tumbaku na pombe, pia dawa zilizothibitishwa kwa
maandishi na daktari.Dawa zinazotolewa kwa udhibitisho wa madaktari ni
zile dawa za kutibu. Pale zinapotolewa kwa sababu nyingine mbali na
matibabu au maelezo ya daktari, zinakuwa dawa za kulevya.Miongoni mwa
dawa zinazotumika vibaya hapa Tanzania nivalium, asprin na panado.
Vimiminika kama petroli pia hutumiwakama dawa za kulevya. Vitu hivi
hutumiwa kwa njia ya kuvuta hewa yake kwa pua au mdomo.Pia kuna vileo
visivyoruhusiwa ambavyo hutengenezwa kienyeji kama vile gongo. Dawa za
kulevya ambazo hutumika sana.Tanzania ni pamoja na bangi, mirungi,
mandrax, heroini na kokaini. Kokaini ambayo hupatikana katika hali ya
ungaunga ulio mweupe, hutumiwa kwa njia ya kuvuta kwa pua au
kuchanganywa na maji na baadaye kujidunga mwilini kwa kutumia
sindano.Heroini pia hupatikana kama unga mweupe. Unaweza kuvuta heroini
kama sigara au kuvuta hewa yake kwa ndani na pia kwa kujidunga sindano.
Katika hali isiyo ya kawaida heroini vilevile inaweza kupatikana katika
vipande vidogovidogo vya kahawia vijulikanavyo kama “sukari ya
kahawia”.Njia nyingine ya kuzungumzia dawa za kulevya ni kutokanana
madhara yake. Yapo madawa ambayo hupagawisha au yanayozubaisha au
kupoozesha kama vile kileo, nikotini, dawa za usingizi, kwa mfano valium
na heroini. Dawa hizo zinamfanya mtumiaji kujisikia shwari, lakini pia
huhuzunisha. Dawa zinazochangamsha ni kama mirungi, kokaini na zile za
kuvuta,kwa mfano petroli, zina madhara ya kukufanya uhamasike na
kujisikia kuwa na nguvu. Dawa zinazopagawisha zinaleta hisia,sauti,
taswira, harufu kwa mtu japokuwa vyote hivyo havipo kweli. Bangi ni
mojawapo ya dawa hizi.
0 comments: