OMMY DIMPOZ KUACHIA NYIMBO MPYA (KOIKOI)
NYOTA wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Omary Faraji ‘Ommy Dimpoz’ ameachia kibao chake kipya kinachokwenda kwa
jina la ‘Koikoi’.
Akizungumza na Habari Mseto jijini
Dar es Salaam, Ommy amesema anaamini wimbo huo utapokelewa vizuri na mashabiki
wake kutokana na mashairi ya wimbo huo ni ya kuburudisha jamii inayomzunguka.
“Namshukuru mungu kazi zangu zote
zinapokelewa vizuri na mashabiki wangu, hivyo nimejipanga kutoa burudani
iliyokwenda shule kwa kutumia kipaji changu ikiwa ni njia moja wapo ya kujivutia
mashabiki wa kutosha,” amesema Ommy Dimpoz.
Amesema anawaomba mashabiki na
wapenzi wa kazi zake wakae mkao wa kula kwaajili ya kuipokea video ya kazi hiyo
ambayo anatarajia kwenda kuitengeneza nje ya nchi.
Ommy Dimpoz kwasasa anatamba na
nyimbo zake kama, Nai nai na Baadae ambazo zilimtambulisha na zinaendelea
kufanya vizuri katika tasnia ya muziki wa bongo fleva.
Na Elizabeth John Kutoka burudan.blogspot.com
0 comments: