TOURE MCHEZAJI BORA AFRIKA MWAKA HUU
Mcheza kiungo wa Manchester City Yaya Toure
ametangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora barani Afrika kwa
mwaka wa pili mfululizo.
Toure alimshinda noadha wa Ivory Coast na
mshambulizi wa zamani wa Chelsea Didier Drogba na aliyekuwa mlinda lango
wa Arsenal Alex Song.Drogba alimaliza katika nafasi ya pili naye Song akawa wa tatu, katika uteuzi uliofanywa na makocha na maafisa wa kiufundi wa timu za soka barani Afrika ambazo ni wanachama wa shirikisho la mchezo wa soka barani Afrika CAF.
Aliyekuwa mshambulizi wa Barcelona Samuel Eto'o ndiye anayeshikilia rekodi ya kushinda tuzo hiyo mara nyingi.
Mabingwa wa soka barani Afrika, Zambia walituzwa kuwa timu bora barani mwaka huu na kocha wao Herve Renard naye aliteuliwa kuwa kocha wa mwaka.
Song kwa sasa anaicheza klabu ya Barcelona naye Drogba anaicheza klabu ya Shanghai Shenhua ya Uchina tangu mwezi Mei Mwaka huu.
Toure, ambaye alishinda tuzo hiyo mwaka uliopita, ni miongoni ma wachezaji wa timu ya taifa ya Ivory Coast, wanaoelekea nchini Afrika Kusini mwa michuano ya kombe la Mataifa Bingwa Barano Afrika itakayoanza mwezi ujao.
0 comments: