JUSTIN BIEBER KUZOMEWA NA MASHABIKI..
Mashabiki wa Justin Bieber wameamua kufika mwisho sasa, walichukulia poa alipoonekana akitembea kifua wazi mitaa ya London licha kuwa ni baridi, walichukulia poa pia waliposkia anavuta bangi, lakini alipokuja kwenye show masaa mawili baadae, waliona sasa amezidi na
kuamua kumchenjia na kumzomea jukwaani
show ya Justin iliyofanyika London siku ya jumatatu, ilitakiwa kuanza saa mbili na nusu usiku, haikufanikiwa kuanza time hiyo baada ya Justin kupanda stage saa nne na nusu usiku, ikiwa amechelewa masaa mawili
Bieber alijaribu kujitetea kuchelewa kwake kwa kuandika kupita mtandao wa twitter kuwa alichelewa kwa dakika 40 tu kwasababu opening acts ilipangwa kufanyika kwa saa moja.
mwisho wa siku alikubali kuwa hakuna utetezi pale ambapo anakua amechelewa, kuchelewa ni kuchelewa tu, na kuilaumu media kwa kusambaza maneno juu ya uzembe wake
0 comments: