Sunday, October 14, 2012

0

2FACE NA D'BANJ KUACHIA NYIMBO MPYA....

Kolabo ya kwanza ya kihistoria inayosubiriwa kati ya wasanii nyota 2Face na D'Banj wa Nigeria, habari ni kwamba wawili hao wanatarajia kuwaongoza wanamuziki nyota barani Afrika katika tamasha la 'Top10mics'.

Tamasha hilo kubwa ambalo litafanyika mwishoni mwa mwezi Novemba katika moja ya hoteli maarufu iliyopo Victoria Island, mjini Lagos Nigeria, litatumbuizwa na nyota Femi Kuti, Flavour na Sir Shina Peters.

Aidha msanii D'Banji anayetesa na kibao chake cha ‘Oliver’ yupo mbioni kutoa albamu yake ya nne iitwayo ‘Mr Endowed’ ambapo hivi sasa wawili hao wamekwishafanya shooting ya video yao mpya ‘Feeling Good’ iliyotayarishwa na Don Jazzy.

Download audio here;

Hulk Share - Music Distribution Platform


0 comments: