Tuesday, October 2, 2012

0

AMINI KUMTAMBURISHA MPENZI WAKE SIKU YA FIESTA YA DAR ES SALAAM TAREHE 06

BAADA ya kusumbuka sana na mapenzi yakiwemo ya kumpenda staa, msanii Amini Mwinyimkuu

‘Amini’, ameuambia mtandao wa DarTalk, kuwa Octoba 6 mwaka huu siku ya tamasha la Fiesta,

atamtambulisha mpenzi wake ambaye, anayechukua nafasi iliyoachwa wazi na Linah.

Kwa hakika utambulisuho huo utakuwa wa aina yake kwani mashabiki wake wengi wanajua jamaa bado

anamzimia Ndege Mnana huku wakiwa hawaelewi kitu kilichowafanya hadi wakaachana ingawa bado

wana mahusiano mazuri kwenye kazi.

Amini aliumpa mtandao huu mchongo huo ili kuwataliafu mashabiki wake kuwa alikuwa kimya kwenye

suala zima la mapenzi baada ya kuumizwa sana, lakini sasa anaamini ni wakati muafaka wa

kumtambulisha kimwana wake.

Alisema kuwa mpenzi atakayemtambulisha siku hiyo ndiye mke mtarajiwa kwani haoni sababu ya

kuendelea kuumizwa na mapenzi wakati muda wa kuvuta jiko umekaribia.

“Sihitaji kumtambilisha kama mpenzi bali ni kama mke kwa sababu naamini anavyonipenda ni kiasi cha

kujivunia kwa sababu mara zote huwa nazungumza naye mambo ya ndoa na yupo radhi kuishi na mimi

kwa shida na raha,” alisema Amini.

From DARTAKL


0 comments: