Thursday, October 18, 2012

0

MATRETKA KUKABIZIWA VIJIJI VYA RUANGWA

.Mkuu wa wilaya ya Ruangwa Bi Agness Hokororo(Mb) akijaribu kabla ya kukabidhi trekta na mkataba wa umiliki wa Trekta hiyo kwa Mwenyekiti wa kijiji cha Chilangalile kata ya Makanjiro,Bw Juma saidi Nangolingo huku ikishuhudiwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw Reubern Mfune katika hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika mbele ya ofisi ya Idara ya Kilimo Wilayani Ruangwa

Wananchi wakishuhudia makabidhiano hayo. Ruangwa

Jumla ya hekta 14960 zinatarajiwa kulimwa wilayani Ruangwa Msimu huu wa kilimo 2012/13 kufuatia upatikananji wa matrekta makubwa yaliyotolewa na Halmashauri hiyo na kukabidhiwa kwa vijiji Vinne vilivyopo Wilayani Humo.

Hayo yalielezwa na Mkuu wa wilaya ya Ruangwa,Bi Agness Hokororo(Mb)alipokuwa akikabidhi trekta 4 aina ya Farmtrac (70E 60 HP 2WD)zilizonunuliwa Kupitia Mpango wa Maendeleo na Uendelezaji Kilimo wilayani(DADPS)Yenye thamani ya Tshs 160 Milioni ikiwa ni gharama ya Ununuzi na Usafirishaji hadi kufika wilayani humo.

Akiongea na Wakulima hao baada ya Taarifa fupi ya makabidhiano iliyosomwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bw Reubern Mfune,Mkuu wa wilaya aliwataka wakulima hao kuanzisha akaunti maalum ya kuyatunza matrekta hayo na mapato yote kuwekwa katika akaunti hizo ili kusaidia kumudu kujiendesha ikiwa pamoja na kuchangia asilimia 20 kwa ajili ya marejesho ya ununuzi wa trekta hizo ili kijiji kiweze kumilikishwa.

Aidha Bi Hokororo aliitaka halmashauri hiyo kupitia maafisa Ugani kuhakikisha wanasaidia uendeshaji wa miradi hiyo huku wakiamasisha Jamii kuandaa mashamba yao ili yasiwe na Visiki ikiwa pamoja na kuhakikisha trekta hizo zinabeba mzigo uliolingana na uwezo uliopangwa kubebwa na trekta hizo.

‘’Nataka muhakikishe kuwa trekta hizo ninazowakabidhi leo zinatumika kwa misingi ya kilimo na ziendeshwe na dereva mwenye leseni na aliepatiwa Mafunzo na si Vinginevyo’’’Alimalizia Hokororo.

Vijiji vilivyonufaika na Mpango huo ni Litama,Nachinyimba,Chilangalile na Michenga ambazo ziliwezeshwa kuibua miradi ya Kilimo na kupatiwa Mafunzo



0 comments: