Monday, January 21, 2013

0

Mhe. January Makamba akutana na Wafanyakazi wa TTCL jijini Dar leo na kusikiliza kero zao


Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba akizungumza na wafanyakazi wa TTCL wakati wa Mkutano wa kutoa kero zao kuhusu Hali mbaya inayoikabiri Kampuni ya Simu ya TTCL na migogoro iliyopo kwenye Kampuni ya hiyo. Mkutano huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya TTCL,Said Amir Said (kushoto) akitoa muongozo kwa wafanyakazi wa TTCL wakati wa Mkutano wa kutoa kero zao kuhusu Hali mbaya inayoikabiri Kampuni hiyo ya TTCL na migogoro iliyopo,uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TTCL,Karim Bablia akitoa kero mbali mbali alizokumbana nazo kwenye kampuni hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba (hayupo pichani) wakati wa Mkutano wa kutoa kero zao kuhusu Hali mbaya inayoikabiri Kampuni hiyo na migogoro iliyopo,uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba,Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu ya TTCL,Said Amir Said pamoja na Mkurugenzi wa Fedha wa TTCL,Shaban Mrisho wakisikiliza kwa makini kero mbali mbali zilizokuwa zikiwasilishwa na wafanyakazi wa TTCL jijini Dar es Salaam,leo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu ya TTCL jijini Dar es Salaam na Wafanyakazi wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia wakifatilia Mkutano huo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,Mhe. January Makamba akiendelea kuongea na Wafanyakazi wa TTCL jijini Dar es Salaam leo.

KWA PICHA ZAIDI TEMBELEA 
http://othmanmichuzi.blogspot.com

0 comments: