TUZO ZA KILI 2013 KURUSHWA LIVE KWENYE INTERNET
Usiku wa Tuzo za Muzizki Tanzania maarufu kama Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 unatarajiwa kuonyeshwa live mtandaoni siku ya Jumamosi, Juni 8. Tofauti na miaka mingine ambayo tukio la utoaji tuzo tu ndio lilikuwa likionyeshwa kupitia kwenye TV pekee, na kuwanyima fursa Watanzania waishio nje ya nchi kufuatilia moja kwa moja, mwaka huu watumiaji wa mtandano waka mwanzo tu Internet wataweza kuangalia tukio la Red Carpet litakaloanza saa moja jioni wakati wanamuziki na wageni waalikwa wakiwasili ukumbini.
Pia tukio la utoaji tuzo litakaloanza rasmi saa tatu usiku litakuwa moja kwa moja mtandaoni hadi litakapofikia mwisho. Watumiaji wa simu za Android, Blackberry, iPhone na tablets wanaweza ku-download application ya LIVESTREAM itakayowawezesha kuangalia moja kwa moja kwenye simu zao wakati watumiaji wa computer watatazama kupitia http://new.livestream.com/KTMA2013 na katika Blogs mbalimbali.
Pia picha za matukio yatakayokuwa yakijiri ukumbini zitapatikana kupitia ukurasa wa Instagram wa kilimanjaro Premium Lager ambo ni www.instagram.com/kili_lager wakati ule wa Twitter www.twitter.com/kili_lager utakuwa ukitoa habari zinazoendelea na washindi wa tuzo na itapatikana pia katika ukurasa wa Facebook wa Kilimanjaro Premium Lager.
0 comments: