Friday, June 7, 2013

0

Neymar asajaliwa na Barcelona



Klabu ya Barcelona, imekubali kumsajili mshambuliaji matata kutoka Brazil Neymar kutoka kwa klabu ya Santos.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, anatarajia kukamilisha uasajili huo siku ya
Jumatatu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Barcelona, vilabu hivyo viwili vimeafikiana kuhusu usajili wa mchezaji huyo.

Barcelona imemtaja mshambuliaji huyo kama mchezaji ambaye ana uwezo wa kuwa bora zaidi duniani.

Katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram, Neymar, alichapisha ripoti kuthibitisha usajili huo na kuwashukuru mashabiki wa Santos, kwa kumuunga mkono katika kipindi cha miaka tisa iliyopita.

Katika taarifa hiyo iliyoandikwa kwa lugha ya Kireno, Neymar, alisema licha ya kuondoka daima moyo wake utasilia na klabu hiyo.

Awali kulikuwa na fununu kuwa klabu ya Real Madrid, vile vile ilikuwa na nia ya kumsajili mchezaji huyo ambaye mkataba wake na Santos ungemalizika msimu ujao.

Neymar atachecheza mechi yake ya mwisho siku ya Jumapili dhidi ya Flamengo, kabla ya kujiunga na Bercelona baada ya fainali za kombe la Shirikisho, ambayo itachezwa kuanzia tarehe kumi na tano hadi thelathini mwezi ujao nchini Brazil.

Katika habari zingine, mshambuliaji matata wa Manchester City Sergio Aquero, amesaini mkataba mpya ambao utaongeza muda wake kwa mwaka mmoja zaidi.

Mchezaji huyo kutoka Argentina ambaye alisaini mkataba wa miaka mitano mwaka wa 2011, kutoka kwa klabu ya Atletico Madrid sasa atasalia na Manchester City hadi mwaka wa 2017.

Aguero ndiye aliyefunga bao lililoifanya Manchester City kunyakuwa kombe la ligi kuu mwaka uliopita wakati walipokuwa wakichuana na QPR

0 comments: